DKT. SAMIA AAHIDI HUDUMA BORA ZA KIJAMII WILAYANI URAMBO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 11, 2025

DKT. SAMIA AAHIDI HUDUMA BORA ZA KIJAMII WILAYANI URAMBO


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza maendeleo katika Wilaya ya Urambo kupitia miradi mikubwa ya afya, elimu, maji, kilimo, na miundombinu.

Akizungumza katika kampeni za uchaguzi mkuu wa 2025, Dkt. Samia amebainisha kwamba ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri umekamilika na huduma za matibabu zimeimarika, ikiwemo huduma 32 muhimu za afya. Aidha, miundombinu ya elimu inaendelea kuboreshwa kwa ujenzi wa vyumba 350 vya madarasa ya shule za msingi na sekondari, pamoja na Shule ya Msingi yenye mtaala wa Kiingereza. Pia, Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kimepangwa kujengwa ili kukuza ufundi stadi miongoni mwa vijana.

Dkt. Samia ameongeza kuwa huduma za maji safi na salama zinaendelea kupanuliwa kupitia miradi ya upatikanaji na usambazaji wa maji, ikiwemo upanuzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria na uchimbaji wa visima vipya. Aidha, katika sekta ya kilimo, kuimarika kwa upatikanaji wa mbolea ya ruzuku kunatarajiwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Kuhusiana na miundombinu, Dkt. Samia ameahidi ujenzi wa barabara za lami, matengenezo ya barabara za changarawe, ujenzi wa soko la kisasa, bwawa na skimu za umwagiliaji, pamoja na hoteli ya kisasa na vibanda vya stendi kuu ya mabasi. Ahadi hizi ni sehemu ya mpango wa maendeleo unaolenga kuinua kipato cha wananchi na kuboresha maisha yao kwa ujumla.





No comments:

Post a Comment