
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM amesema ikiwa atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, atajenga madaraja 133 ndani ya Mkoa wa Tabora pamoja na barabara mbalimbali za Kimkakati.
Akizungumza na maelfu ya wananchi wa Tabora Mjini kwenye viwanja vya Ipuli leo Septemba 12, 2025, Dkt. Samia pia ameahidi kuweka taa 2300 Mkoani humo ikiwa atachaguliwa ili kuruhusu shughuli za kiuchumi kufanyika kwa muda wote.
"Tabora na Wilaya za Tabora zitapata fursa ya kufanya biashara kwa masaa 24 kwasababu umeme ni usalama, umeme ni mwanga na unasaidia kwenye uzalishaji na tunapoweka taa tunatoa fursa Vijana wetu hawa wafanye kazi kwa saa 24." Amekaririwa akisema Dkt. Samia.
Dkt. Samia amemaliza kampeni zake Mkoani Tabora ambapo kama ilivyokuwa kwenye Mikoa mingine ametumia Mikutano yake kueleza mafanikio yake kwenye kipindi cha Miaka minne na nusu aliyoongoza pamoja na ahadi zake mbalimbali ambazo atazifanya kwa miaka mitano ijayo ikiwa atachaguliwa Oktoba 29, 2025.





No comments:
Post a Comment