
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Septemba 30, 2025 anatarajiwa kuwa na mikutano ya Kampeni kwenye Wilaya ya Korogwe pamoja na Mombo mkoani Tanga na baadae kuingia Mkoani Kilimanjaro kwenye Wilaya za Same na Mwanga.
Dkt. Samia ananadi Ilani ya Chama chake, Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2025/30, kuomba kura pamoja na kueleza mafanikio ya serikali yake ya awamu ya sita, akiwanadi pia wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani kwenye Wilaya anazofika, akiwa mwanamke wa kwanza kuwania nafasi hiyo katika historia ya Chama hicho, miongoni mwa Vyama vikongwe na vilivyokaa madarakani muda mrefu zaidi barani Afrika.
Akiwa Mkoani Tanga jana Jumatatu, Dkt. Samia ameahidi utekelezaji wa mradi wa reli ya kisasa ambayo itaunganishwa na bandari ya Tanga kuelekea Arusha hadi Musoma ikiwa na urefu wa Kilomita 1.108 pamoja na kufanya upanuzi na ukarabati wa barabara ya Dar Es Salaam- Chalinze- Segera- Arusha (Km 646) ili kuondoa changamoto ya msongamano kwenye barabara hiyo muhimu na kuu kwa ukanda wa Kaskazini.
"Mwelekeo wetu kwa ujumla ni kuirejesha ile Tanga ya Viwanda kama sehemu ya mkakati wa Kitaifa wa kuijenga Tanzania ya Viwanda kwa kuanzisha na kuendeleza kongani za Viwanda katika kila Wilaya. Sambamba na hilo tumedhamiria pia kufufua viwanda vilivyobinafsishwa lakini havijaendelezwa ikiwemo kiwanda cha chai Korogwe." Amesisitiza Dkt. Samia.
Katika Ilani Ijayo anayoinadi Dkt. Samia, CCM imeahidi kwa Wilaya ya Mwanga kujenga kituo cha afya Chomvu, ujenzi wa Zahanati ya Kimbale na Masumbeni,kujenga kwa kiwango cha lamk barabara za Kikwenj- Vuchama, Kisangara-Shighatinj, Usangi-Kwakindi, Ujenzi wa soko la mazao Kituri, utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji ikiwemo Masumbeni, Kadengere, Ubembe- Kitiriko, Nyumba ya Mungu, Mwai, Mangio, Mwaniko na Lambo, Kileo, Kivulini pamoja na mradi wa maji Kimbale.
Kwa Same Dkt. Samia kupitia Ilani anayoinadi wameahidi kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Same, ujenzi wa barabara mbalimbali ikiwemo za Mji wa Same kwa kiwango cha lami pamoja na za changarawe ikiwemo barabara ya John Malecela- Makanya- Ruvu, Kwa Same Dkt. Samia kupitia Ilani anayoinadi wameahidi kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Same, ujenzi wa barabara mbalimbali ikiwemo za Mji wa Same kwa kiwango cha lami pamoja na za changarawe ikiwemo barabara ya John Malecela- Makanya- Ruvu, ukamilishaji wa miradi ya maji ya Mroyo, Vuje, Kihurio, Msindo, Maore- Baseline- Ihindi pamoja na Kirore sambamba na kujenga na kukarabati skimu mbalimbali za umwagiliaji Wilayani humo.

No comments:
Post a Comment