
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Septemba 17, 2025 akiwa kwenye Mkutano wake wa kwanza wa Kampeni Makunduchi Kisiwani Unguja, Zanzibar. Dkt. Samia ambaye chimbuko lake ni Zanzibar ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na wa kwanza kusimamishwa na Chama Cha Mapinduzi CCM kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania, akiwa Mwanamke wa kwanza pia kuwa Rais wa Tanzania baada ya kuchukua nafasi ya Mtangulizi wake Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mwaka 2021.




No comments:
Post a Comment