THBUB YAWATAHADHARISHA WAANDISHI JUU YA MATUMIZI MABAYA YA MAJUKWAA YA HABARI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, September 17, 2025

THBUB YAWATAHADHARISHA WAANDISHI JUU YA MATUMIZI MABAYA YA MAJUKWAA YA HABARI

 

Na Gideon Gregory, Dodoma 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), inatoa wito kwa Waandishi wa Habari kuchukua tahadhari dhidi ya matumizi mabaya ya majukwaa ya habari ikiwemo mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vijikite katika kuimarisha amani, utulivu na demokrasia nchini kwa kutotumika vibaya kalamu zao.

‎Wito huo umetolewa leo Septemba 17,2025  katika Ukumbi wa Hotel ya Mesuma Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu wakati akifungua mafunzo kwa Waandishi wa Habari  kuhusu uzingatiwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora katika mchakato wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29,2025. 

‎"Katika kipindi hiki cha uchaguzi, Waandishi wa Habari  wanao wajibu wa kuripoti matukio yote ya uchaguzi kwa usahihi bila upendeleo wowote wa Chama, Mgombea au msimamo wowote wa Kisiasa na kuweka uwiano sawia wa taarifa kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi", amesema.

‎Aidha, amewataka waandishi wa habari, kutumia mbinu madhubuti kwenye majukwaa ya kidigitali na vyombo vingine vya Habari ili kuepusha upotoshaji wa taarifa binafsi au kusema uongo juu ya Mgombea.

Mbali na hayo, Jaji mstaafu, Mathew Mwaimu, ametoa rai kwa Waandishi wa Habari, kuepuka kuchapisha au kutangaza habari zenye nia ya kuchochea vurugu, ubaguzi, chuki za Kisiasa kikabila, kidini na kijinsia.

‎"Nitoe wito kwa Waandishi wa Habari, kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya Kijamii, na vyombo vya Habari vijikite katika kuimarisha amani, utulivu na demokrasia nchini,"amesema. 

Amesema mafunzo hayo yatawasaidia waandishi wa habari kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zilizowekwa ili kuepukama ma migongano baina ya vyombo vya dola na waandishi wa habari wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

"Pia mafunzo haya yataongeza uelewa kwa waandishi wa habari kuhusu haki na wajibu wao wakati Wanapotekeleza majukumu yao katika kipindi chote cha uchaguzi hii itasaidia kuwepo na uhuru wa habari na uhuru wa vyombo vya habari,"amesema. 

‎Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (DPC), Blaya Moses, amewataka waandishi wa Habari kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni na miongozo ya kiuandishi ili kujiepusha na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza. 






No comments:

Post a Comment