MAWAKILI WATAKIWA KUJITOA KUTOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, September 17, 2025

MAWAKILI WATAKIWA KUJITOA KUTOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA


Mawakili wa kujitegemea wametakiwa kujitoa kwa moyo kutoa Huduma za Msaada wa Kisheria kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa Taifa sambamba na kuwa waadilifu katika kushughulikia migogoro ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanashughulikia migogoro hiyo mpaka mwisho na kutoa taaraifa za kila hatua ya kushughulikia migogoro hiyo ili kujenga Imani kwa wananchi.

Wito huo umetolewa leo, Septemba 17, 2025 na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Rwezimula anayemuwakilisha Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Ndg. Eliakim Maswi katika ufunguzi wa Mafunzo kwa Mawakili wa Kujitegemea kwa ajili ya utoaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria yanayofanyika katika Ukumbi wa Morena Hoteli mkoani Morogoro.

Maswi amewataka washiriki kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo na kuwa huru kujadili na kuuliza maswali kwa kuwa uelewa watakaoupata utawasaidia kuboresha Huduma za Msaada wa Kisheria na kuwa chanzo cha upatikanaji haki kwa wananchi wasiojiweza na waliopembezoni wanaoshindwa kufikia huduma kwa haraka na kupelekea kupoteza haki zao.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Ester Msambazi alisema kuwa mafunzo haya yanalenga kujadili namna ya kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi wasio na uwezo na wale walio pembezoni ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma za mawakili kwa wananchi hao.

“Tutakumbushana pia miiko ya utendaji kazi na wajibu wetu Pamoja na kukubaliana maeneo ya kuwafanyia kazi ili kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi na kuwa chachu kubwa ya mabadiliko yanayohusiana na masuala ya upatikanaji haki katika jamii’’ alisisitiza Msambazi.

Kwa uapnde wake mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani , Rose Nyatega alisema kuwa GIZ inashirikiana na wadau na Serikali kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa wananchi wote ili kuboresha Utawala Bora, Haki za Binadamu pamoja na Usawa wa Kijinsia.





No comments:

Post a Comment