Eng Samamba Awataka Wadau wa Sekta ya Madini Kutumia Maonesho ya Geita Kuelimisha Wananchi - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, September 22, 2025

Eng Samamba Awataka Wadau wa Sekta ya Madini Kutumia Maonesho ya Geita Kuelimisha Wananchi



Na Mwandishi Wetu, Geita


Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, amewataka wadau wa Sekta ya Madini kutumia vyema fursa ya Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini Geita yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Bombamlbili kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya mambo muhimu ya sekta hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda ya Wizara ya Madini, taasisi zake na wadau mbalimbali, Mhandisi Samamba amesema maonesho hayo si tu jukwaa la kuonesha bidhaa na teknolojia, bali pia ni sehemu ya kuwafikia wananchi kwa elimu na taarifa sahihi zinazohusu sekta ya madini.

“Wananchi wakielimishwa vizuri watashiriki kwa uelewa, watafaidika zaidi na rasilimali hizi na kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusimamia sekta hii,” amesema Samamba.

Aidha, Mhandisi Samamba amewapongeza washiriki wote kwa ushiriki wao na kuwasisitiza kuendelea kuonesha nafasi ya Sekta ya Madini katika kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa na maisha ya Watanzania.

Pia, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo ametembelea mabanda hayo na kupata maelezo kutoka kwa wadau mbalimbali wa madini, maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa hivi punde na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.



No comments:

Post a Comment