MIRADI YA MAENDELEO MKOANI RUVUMA NI KIELELEZO CHA DHAMIRA NJEMA YA CCM- DKT. SAMIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, September 22, 2025

MIRADI YA MAENDELEO MKOANI RUVUMA NI KIELELEZO CHA DHAMIRA NJEMA YA CCM- DKT. SAMIA


Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema utekelezaji wa miradi mikubwa ya afya, elimu, maji na barabara katika wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma ni kielelezo halisi cha dhamira ya serikali inayoundwa na Chama Cha Mapinduzi katika kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka na yenye tija kaa kila mmoja.

Dkt. Samia ameyaeleza hayo leo Jumatatu Septemba 22, 2025 Mjini Tunduma kwenye Kampeni zake kwenye uwanja wa CCM Nanjoka kwenye muendelezo wa Kampeni za uchaguzi Mkuu, akisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imekamilisha ujenzi wa zahanati zaidi ya 15 na vituo vya afya vipya ikiwemo Vituo vya afua Jakika, Namiungo na Mindu, sambamba na kukamilisha majengo ya kujifungulia akina mama na vitengo vya dharura kwenye Hospitali ya Wilaya ya Tunduru.

Aidha, Mgombea huyo amesema katika kipindi hicho huduma za elimu zimeimarishwa kwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa zaidi ya 200, maabara 10 na shule mpya za sekondari, pamoja na ujenzi wa hosteli na mabweni ili wanafunzi wapate fursa sawa za kusoma bila vikwazo.

Katika sekta ya miundombinu, Dkt. Samia ametaja ujenzi wa barabara ya Mtwarapachani–Nalasi–Tunduru yenye urefu wa km 318 kwa kiwango cha lami, pamoja na daraja la Ngapa lenye urefu wa mita 55, kama hatua inayofungua njia za biashara na usafirishaji wa mazao.

Ameongeza kuwa miradi ya maji safi na salama imeendelea kupanuliwa kupitia uchimbaji wa visima, mabwawa na miradi ya kusambaza maji kwenye vijiji vya Nalasi, Ligunga, Namwinyu na Nampungu, hatua inayopunguza adha ya akina mama na watoto kusaka maji kwa umbali mrefu.

Katika upande wa biashara na ajira, Dkt. Samia ambaye ni Mgombea wa kwanza mwanamke kuwahi kuteuliwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi kuwania nafasi hiyo, amesema ujenzi wa soko la kisasa mjini Tunduru na ukumbi wa kisasa wa wilaya (Multipurpose Hall) unakusudiwa kuinua uchumi wa wananchi na kutoa nafasi kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa kunufaika.

“Tumefanikisha mengi Tunduru: afya bora, elimu yenye mazingira mazuri, barabara za kisasa na huduma za maji kwa wananchi. Lakini bado tunataka kuongeza kasi ili kila kijiji kifikwe na huduma hizi. Hii ndiyo dhamira ya CCM,” amesema Dkt. Samia.



No comments:

Post a Comment