SENYAMULE : MADEREVA SERIKALINI ZIANGATIENI SHERIA KUPUNGUZA AJALI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, September 5, 2025

SENYAMULE : MADEREVA SERIKALINI ZIANGATIENI SHERIA KUPUNGUZA AJALI


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ametoa wito kwa Madereva wa Serikali kuwa makini wakati wakitimiza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria ili kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, ulemavu na kuisababishia Serikali hasara kubwa.

Amesema hayo Septemba 04, 2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma wakati akifunga Kongamano la Nne la Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST).

Amewasisitiza madereva kutumia mafunzo mbalimbali yaliyotolewa katika Kongamano hilo kupitia mada mbalimbali zilizowasilishwa na Wakufunzi kuboresha uwezo wao katika utendaji wao wa kazi.

Aidha, Senyamule ametoa pongezi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja na kuweka taa za mwanga ambazo zinasaidia usalama wa Madereva na Raia nyakati za usiku.

Vilevile, Ametoa pongezi kwa Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya madereva wa Serikali ikiwemo ongezeko la vitendea kazi ikiwemo ununuzi wa magari ya kisasa na hivyo kupelekea vijana kupata ajira nyingi Serikalini


Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde amekipongeza Chama hicho kwa kuendelea kuongeza idadi ya washiriki katika Makongamano kutoka washiriki 400 hadi kufikia 2,500 ambapo Makongamano hayo yamekuwa yakisaidia kuwajengea madereva wa Serikali umahiri na uweledi mahala pa kazi.




Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST), Said Kapande amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Chama hicho mpaka sasa kuna mafanikio mbalimbali yamepatikana ikiwemo kuanzishwa ofisi Zanzibar kwa ajili ya kuimarisha mshikamano wanachama wa
Zanzibar pamoja na Kuongeza wanachama wa Zanzibar kutoka 150 hadi 260 kuunganishwa na Chama cha Tanzania Bara.


Kongamano la Nne la Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania limefungwa leo likiwa limehudhuriwa na washiriki takibran madereva 3,500 na kubebwa na kauli mbiu “Dereva wa Serikali “Epuka ajali, linda gari lako na watumiaji wengine wa barabara, Shiriki Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba 2025 ”






No comments:

Post a Comment