SWAHIBA MJENZI KUONGEZA THAMANI LIGI YA MKOA WA DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, September 19, 2025

SWAHIBA MJENZI KUONGEZA THAMANI LIGI YA MKOA WA DODOMA



Na Mwandishi Wetu, Dodoma


Ligi ya mpira wa miguu mkoa wa Dodoma inatarajiwa kuanza rasmi Septemba 27, ikikutanisha timu 16 mbalimbali kutoka wilaya zote za mkoa huo zitashiriki.

Ligi hiyo ambayo hufanyika kila mwaka inalenga kuinua vipaji vya wachezaji chipukizi pamoja na kuongeza hamasa ya michezo katika jamii ya Dodoma.

Akizungumza na wanahabari leo Septemba 19,2025 Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA), CPA Edwin Michael amesema maandalizi yote muhimu yamekamilika, ikiwemo upangaji wa ratiba, maandalizi ya viwanja na usajili wa wachezaji.

"Mashindano ya mwaka huu tunataka kidogo yafanyike kwa utofauti, kwanza itambulike kuwa mkoa huu unacheza ligi lakini sio kucheza tu ligi na watu wahamasike kidogo kuja kutazama mechi zetu mbalimbali na tumeweka kwenye mtindo tofauti kidogo na miaka mingine ambapo mashindano haya kwa miaka mingine yalikuwa yanafanyika kwa vituo mbalimbali ambavyo saa zingine yalikuwa yanazinyima fursa timu zingine sana sana timu mwenyeji angalau kuweza kushuhudia timu yao ikicheza,"amesema.

Ameutaja mtindo wa mwaka huu kuwa, ligi hiyo itachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini katika makundi ambapo utatoa fursa kwa timu washiriki kuweza kuhamasika kushirikiana na washirika wao ili kuendesha hizo timu.

"Mashindano haya yanashirikisha vijana chini ya miaka 20, huo ndio msisitizo kama ilivyoletwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), lengo ni kukuza vipaji vya vijana, ndiyo maana ligi hii imetoka kwenye mtindo ule wa kuchukua wachezaji wa ngazi yoyote lakini inataka vijana wacheze ligi hii,"amesema.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa kamati ya mashindano DOREFA Mohamed Abdallah amesema ligi hiyo itatanguliwa na mchezo wa Ngao ya Hisani utakao wakutanisha timu ya Sheri Sports Center kutoka Dodoma Mjini dhini ya Zabibu FC kutoka Wilaya ya Chamwino katika uwanja wa Sheri Complex majira ya saa Kumi jioni.

"Kabla ya mchezo huu utatanguliwa na michezo mingi ya ufunguzi, kwasababu kutakuwa na bonanza rasmi la DOREFA kwaajili ya ufunguzi wa ligi hii,"amesema. 

Katika kuelekea msimu huo mpya wa ligi ya Mkoa wa Dodoma DOREFA wameingia makubaliano ya mashirikiano ya uendeshaji wa ligi hiyo na Taasisi ya inayounda na kusadifu mashindano mbalimbali ya mpira wa miguu (Swahiba Mjenzi).

Akizungumzia ushirikiano huo Afisa Mtendaji Mkuu wa Swahiba Mjenzi Hamis Makira amesema mashirikiano hayo yanalenga ni kuipa thamani ligi hiyo kwa kuweza kuitangaza.

Mshindi wa ligi ya mkoa atapata nafasi ya kushiriki mashindano ya ngazi ya juu ya kitaifa, hatua inayotarajiwa kuongeza ushindani na kuvutia wadau wengi zaidi.











No comments:

Post a Comment