NA OKULY JULIUS, OKULY BLOG, DODOMA
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) zimesaini hati ya makubaliano ya kubadilishana taarifa (Data Sharing Agreement – DSA), hatua inayolenga kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa na utakatishaji fedha nchini.
Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika leo, Septemba 24, 2025, katika makao makuu ya TAKUKURU jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Francis Chalamila, pamoja na Kamishna wa FIU, Bw. Majaba Shabani Magana, wakurugenzi na maafisa wa taasisi hizo.
Akizungumza katika tukio hilo, Bw. Chalamila alisema makubaliano hayo ni mwendelezo wa ushirikiano wa muda mrefu kati ya taasisi hizo mbili, ulioanzishwa tangu kusainiwa kwa makubaliano ya awali (MoU) mwaka 2015.
“Makubaliano haya mapya ya ubadilishanaji taarifa ni utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Serikali Mtandao ya mwaka 2023, inayozitaka taasisi zinazoshirikiana kuhakikisha zinasaini Data Sharing Agreement endapo zitahusiana katika kubadilishana taarifa,” alisema Bw. Chalamila.
Aliongeza kuwa lengo kuu la makubaliano hayo ni kurahisisha na kuwezesha ubadilishanaji wa taarifa kati ya TAKUKURU na FIU ili kuongeza ufanisi wa uchunguzi na udhibiti wa vitendo vya rushwa na utakatishaji fedha haramu.
Kwa mujibu wa Bw. Chalamila, katika kipindi cha mwaka 2022 hadi 2025, TAKUKURU imepokea taarifa fiche 47 za miamala yenye mashaka kutoka FIU, ambapo 36 kati yake zilianzishiwa uchunguzi. Aidha, kati ya mwaka 2023 hadi 2025, taasisi hiyo iliomba taarifa 141 kutoka FIU kwa ajili ya kusaidia uchunguzi mbalimbali.
“FIU imekuwa msaada mkubwa katika kufanikisha uchunguzi wetu. Ushirikiano huu umewezesha chunguzi kufanyika kwa wepesi na kwa matokeo chanya,” alisisitiza Bw. Chalamila.
Ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana na TAKUKURU ili kufanikisha azma ya taifa ya kupambana na rushwa, akisisitiza kaulimbiu ya taasisi hiyo: “Kuzuia Rushwa ni Jukumu Lako na Langu; Tutimize Wajibu Wetu.”
Kwa upande wake, Kamishna wa FIU, Bw. Magana, alisema hatua hiyo ni muhimu katika kutatua changamoto ya ukosefu wa mfumo wa kitaifa wa kielektroniki wa kuhifadhi takwimu za uhalifu, hali iliyosababisha taarifa za awali kutoendana na hivyo kukwamisha juhudi za kupata taswira kamili ya mwenendo wa uhalifu wa kifedha nchini

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bw.Crispin Chalamila (kushoto) akiwa na Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU), Bw. Majaba Magana (kulia) wakisani hati ya makubaliano ya kubadilishana taarifa (Data Sharing Agreement),hafla iliyofanyika leo Septemba 24,2025 katika makao makuu ya TAKUKURU jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bw.Crispin Chalamila (kushoto) akiwa na Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU), Bw. Majaba Magana (kulia) wakionesha hati ya makubaliano ya kubadilishana taarifa (Data Sharing Agreement) mara baada ya kusaini Makubaliano hayo ,hafla iliyofanyika leo Septemba 24,2025 katika makao makuu ya TAKUKURU jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bw.Crispin Chalamila (kushoto) akiwa na Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU), Bw. Majaba Magana (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya kubadilishana taarifa (Data Sharing Agreement) mara baada ya kusaini Makubaliano hayo ,hafla iliyofanyika leo Septemba 24,2025 katika makao makuu ya TAKUKURU jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bw.Crispin Chalamila,akizungumza mara baada ya kusaini hati ya ya makubaliano ya kubadilishana taarifa (Data Sharing Agreement) kati ya TAKUKURU na FIU,hafla iliyofanyika leo Septemba 24,2025 katika Makao Makuu ya TAKUKURU jijini Dodoma.

Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU), Bw. Majaba Magana,akizungumza mara baada ya kusaini hati ya Makubaliano ya kubadilishana taarifa (Data Sharing Agreement) kati ya FIU na TAKUKURU ,hafla iliyofanyika leo Septemba 24,2025 katika Makao Makuu ya TAKUKURU jijini Dodoma.


Well done
ReplyDelete