TAKUKURU TANDAHIMBA YAOKOA SH. 500,000/= - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 4, 2025

TAKUKURU TANDAHIMBA YAOKOA SH. 500,000/=


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Wilaya ya Tandahimba imekabidhi fedha TSh. 500,000/= kwa Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Salama, Mwl. Mustafa Shaibu Rashidi, iliyookolewa na TAKUKURU baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Mkupete (W) Tandahimba katika mkutano wa Hadhara uliofanyika Mwezi Aprili, 2025.

Ilielezwa kwenye mkutano huo kwamba wananchi hao walichanga fedha kwa ajili ya kumlipa mwalimu wa somo la Biology na Elimu ya Dini ya Kiislam katika Shule ya Sekondari Salama iliyopo kijijini hapo, lakini Mwl. Lameck Sijaona Kijalo ambaye alikuwa akisimamia ukusanyaji huo, alizitumia fedha hizo kwa manufaa yake binafsi.

Fedha hizo zimekabidhiwa leo katika Shule ya Sekondari Salama na Afisa wa TAKUKURU Bi. Siudhiki Mohamed Joginda, mbele ya wananchi wa Kijiji cha Mkupete.


TAKUKURU (W)TANDAHIMBA Septemba 4 ,2025*

No comments:

Post a Comment