AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITATU AU KULIPA FAINI YA TSH. 300,000/= KWA KUOMBA NA KUPOKEA HONGO YA TSH. 20,000/= - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 18, 2025

AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITATU AU KULIPA FAINI YA TSH. 300,000/= KWA KUOMBA NA KUPOKEA HONGO YA TSH. 20,000/=


NA MWANDISHI WETU - HOLILI, KILIMANJARO


Mnamo Oktoba 15, 2025 katika Mahakama ya Wilaya ya Rombo mbele ya Mhe. Innocent Nyella - Hakimu Mkuu Mwandamizi, imeamriwa kesi ya jinai namba 9081/2025 ikiwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Bw. Hemrod Elias Ngunga - Fundi Bomba wa ROMBOWSSA. Bw. Ngunga alishtakiwa kwa kosa la kushawishi, kuomba na kupokea hongo chini ya vifungu vya 15 (1)(a)(b)( 2) vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya Mwaka 2022.

Mawakili wa Serikali Bi. Furahini Kibanga na Bw. Anold Mafwele wameieleza mahakama kuwa mshtakiwa akiwa Fundi Bomba katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Rombo (ROMBOWSSA) alishawishi, aliomba na kupokea hongo ya kiasi cha Tsh. 20,000/= kutoka kwa mteja ili aweze kumrejeshea mteja mita zake zilizokuwa zimeibiwa maeneo ya Holili.


Mahakama imemkuta mshtakiwa na hatia na kumuamuru kulipa faini ya Tsh. 300,000/= au kwenda jela miaka mitatu, mshtakiwa ameshindwa kulipa faini hivyo amepelekwa rumande.

No comments:

Post a Comment