KISHINDO CHA DKT. SAMIA KUSIKIKA RUKWA NA KATAVI, ASEMA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA YANAWAPA KUJIAMINI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 18, 2025

KISHINDO CHA DKT. SAMIA KUSIKIKA RUKWA NA KATAVI, ASEMA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA YANAWAPA KUJIAMINI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.



Leo hii Jumamosi Oktoba 18, 2025, Dkt. Samia anatarajiwa kuendelea na Kampeni zake kwenye Mikoa ya Katavi na Rukwa ikiwemo Mpanda Mjini, Kibaoni na baadaye Nkasi Kaskazini Mkoani Rukwa, akitumia mikutano hiyo kueleza Ilani ya Chama chake, kuomba kura na kueleza msururu wa mafanikio aliyoyafikia katika kuhudumia watanzania. Amesikika mara zote akieleza kuwa maendeleo ni hatua na ataziongeza zaidi hatua hizo kila wakati kuhakikisha kuwa Watanzania wanastawi na kupata huduma zote muhimu, kwa urahisi na uhakika zaidi.

Ndani ya Miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hatua kubwa za maendeleo zimepigwa. Kwa idadi na takwimu ni dhahiri kuwa katika muda mchache wa kukaa kwake madarakani yapo mambo yenye kuonekana kwa macho na yasiyohitaji hadubini. Mara zote Dkt. Samia anasema mafanikio yaliyopatikana yanampa sababu ya kuamini kuwa hata yaliyopo kwenye Ilani ya sasa yanaweza kutimizwa kikamilifu na kwa wakati.

Miongoni mwa Machache aliyofanikiwa ni pamoja na ongezeko la uzalishaji wa umeme nchini kutoka megawati 1, 602. 32 mwaka 2020 hadi megawati 3, 077. 96 mwaka 2024 kutokana na kukamilika kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, suala ambalo limechochea ukuaji wa shuguli za kiuchumi.

Dkt. Samia pia amefanikisha ujenzi wa vituo vipya 1, 288 vya kutolea huduma za afya ikiwemo Zahanati 947, Vituo vya afya 277, Hospitali za Halmashauri 57, Hospitali za Mikoa 4 na Hospitali 3 za Kanda pamoja na kuimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi ambapo upatikanaji wa dawa muhimu za kipaumbele (aina 290) umefikia asilimia 89.3 ikilinganishwa na asilimia 75.6 mwaka 2020.

Katika sekta ya afya amefanikiwa pia Kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga, Vifo vya akinamama wakati wa uzazi vikipungua kutoka 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2020 hadi vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2024. Vifo vya watoto wachanga vimepungua pia kutoka 67 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2020 hadi kufikia vifo 43 kwa vizazi hai 1,000 mwaka 2024.

Kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma za maji kwa wananchi waishio Vijijini kutoka asilimia 70.1 mwaka 2020 hadi 76.9 na kwa mijini kutoka asilimia 84 hadi 90 mwaka 2024. Ongezeko hilo likichangiwa na kukamilika kwa miradi 1, 633 ya usambazaji maji Vijijini na Mijini, ikiwanufaisha wananchi 12, 547, 526.

Kuongezeka kwa mtandao wa barabara za lami kutoka Kilomita 13, 235.1 mwaka 2020 hadi Kilomita 15, 366. 36. Kuongezeka kwa wigo na idadi ya Watalii na abiria wanaotumia usafiri wa anga kutoka Milioni 2.4 mwaka 2020 hadi Milioni 3.9 mwaka 2024 ikitokana na ununuzi wa ndege mpya ambapo hadi kufikia Oktoba 2024 jumla ya ndege 16 zimenunuliwa na kuongeza safari za ndani na nje ya Tanzania.

Akiwa Mwanamke wa kwanza nchini Tanzania kuwa Makamu wa Rais na baadae Rais wa Tanzania, Jinsi yake na hamasa yake imesaidia pia uongezeka kwa ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi kutoka wanawake 2, 390 mwaka 2020 hadi wanawake 2, 660 mwaka 2024 ikiwemo Mawaziri na Manaibu 10, Mabalozi 8, Wakuu wa Mikoa 7, Makatibu na Manaibu Makatibu 14, Makatibu tawala wa Mikoa 12, Majaji wa mahakama 48, Wakuu wa Wilaya 37, Wabunge 147, Makatibu tawala wa Wilaya 51, Wakurugenzi wa Halmashauri 52, Madiwani 1,604 na Wakuu wa Idara 670 kwenye Halmashauri za Tanzania bara.

No comments:

Post a Comment