CHAMA CHA SIASA KINACHOSUSIA UCHAGUZI NI CHAMA CHA FUJO- WENJE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 18, 2025

CHAMA CHA SIASA KINACHOSUSIA UCHAGUZI NI CHAMA CHA FUJO- WENJE



"Mimi huwa naamini kwasababu biblia inasema ufalme wa mbingu hunyakuliwa na watu wenye nguvu, umati huu ni ushahidi wa nguvu ya Chama Cha Mapinduzi. Mhe. Mwenyekiti (Dkt. Samia Suluhu Hassan) wiki moja iliyopita mimi nilikuwa mwanachama wa Kile chama cha matusi, chama cha malalamiko, Chama cha makasiriko sasa nimepata wokovu mpya na mimi sasa ni mwanachama safi wa Chama Cha Mapinduzi.

Kile Chama kinashinda kwenye mitandao toka asubuhi, mchana na usiku na kazi yao ni kutukana, hawana mipango, hawana mikakati- wamegota. Mimi ninaamini katika taifa tunapaswa kutofautiana kwenye sera za kilimo, afya, maji lakini linapokuja suala la ulinzi na usalama na amani ya nchi yetu hilo ni jambo lisilohitaji mjadala.

"Naamini kila Mtanzania ana wajibu wa kulinda amani ya nchi yetu. Kwahiyo inapotokea leo Chama Cha siasa kinakataa kushiriki uchaguzi maana yake hicho ni kiashiria cha wao kutaka fujo kwasababu mamlaka ya nchi hii na madaraka inapatikana kwenye sanduku la kura tu.

Takwimu hazidanganyi ndugu zangu huko nje kuna watu kazi yao ni kelele tu hakuna maendeleo, wanatupotezea muda tu. Mwaka 2010 mimi nilichaguliwa kuwa Mbunge wa Nyamagana kwa sheria na tume hii hii na kuna wengine wamebaki kwenye hicho Chama na walichaguliwa mara mbili, wengine mara moja, madiwani walipatikana wengi tu. Kipindi wanachaguliwa Tume ya uchaguzi ni huru na ina haki, wananchi wakiwakataa, wakashindwa Tume ni mbaya, Huo ni ujinga. Tulikuja na msemo wa no election, no reforms, ndugu zangu imegota, uchaguzi upo jiandaeni kupiga kura." Ezekiah Wenje, akimnadi Mgombea Urais wa Tanzania kwa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 19, 2025 Mpanda Mkoani Katavi.

No comments:

Post a Comment