DKT. SAMIA AAHIDI KUJENGA MADARAJA NA BARABARA ZA LAMI MANISPAA YA MPANDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 18, 2025

DKT. SAMIA AAHIDI KUJENGA MADARAJA NA BARABARA ZA LAMI MANISPAA YA MPANDA



Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa ndani ya miaka mitano ijayo ikiwa atapewa ridhaa ya kuunda serikali, atajenga madaraja ya Mto Mpanda, lenye kuunganisha Kata za Kakese, Manispaa ya Mpanda na Kata ya Itenka iliyopo Nsimbo Mkoani Katavi, pamoja na ujenzi wa barabara za lami na Changarawe ndani ya Mkoa huo.

Dkt. Samia ametoa ahadi hiyo leo Jumamosi Oktoba 19, 2025 kwenye Viwanja vya Azimio Wilayani Mpanda Mkoani Katavi, akiahidi pia ujenzi wa madaraja mengine ikiwemo madaraja ya Mawe, Manga, Kasokola na Ilembo yaliyopo ndani ya Manispaa ya Mpanda.

Katika hotuba yake Dkt. Samia pia amesema anafahamu uhitaji wa barabara ya Mpanda- Ugala- Kaliua, akiitaja kama barabara muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Katavi na ameahidi kuwa ikiwa atachaguliwa barabara hiyo pamoja na nyingine zilizotajwa kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2025/30, zitakuwa kipaumbele katika utekelezaji wa ahadi zake anazozitoa kwenye Kampeni za uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.


No comments:

Post a Comment