DKT. SAMIA AMEDUMISHA AMANI NA UTULIVU WA TANZANIA- MCH. MSIGWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, October 24, 2025

DKT. SAMIA AMEDUMISHA AMANI NA UTULIVU WA TANZANIA- MCH. MSIGWA


Mbunge wa Zamani wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa amesema ndani ya Miaka minne ya Uongozi wa serikali ya awamu ya sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanikiwa kuendeleza tunu za amani na utulivu nchini ikiwa ni utekeleza wa maono na matamanio ya waasisi wa Tanzania, wakiamini Amani na utulivu ndiyo msingi wa maendeleo.

"Tunu hii ya amani na utulivu imechagizwa vilivyo na Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeiongoza nchi hii kwa ujasiri, kwa maono na malengo ili taifa letu liende mbele. Palipo na magomvi ndoto hazizaliwi, palipo na mafarakano nyimbo haziimbiki, pale penye mafarakano ubunifu unakosekana. Lakini kwasababu tunaye Rais anayeipenda Tanzania ndiyo maana tunu hii imeendelea kusalia nchini." Amekaririwa akisema Mch. Msigwa.

Msigwa amebainisha hayo leo Ijumaa Oktoba 24, 2025 wakati wa Mkutano wa Kampeni za Dkt. Samia Suluhu Hassan huko Unguja Visiwani Zanzibar kwenye viwanja vya Mnazi mmoja, akiwataka Watanzania kuwapuuza wale wote ambao wanadai kuwa CCM na Dkt. Samia hawajali maendeleo ya watu.

Katika maelezo yake pia Mch. Msigwa ametuma ujumbe kwa vijana wa Kitanzania akiwataka kuenzi fikra za waasisi wa Tanzania na kuwakataa wale wote wenye kutenda vitendo vyenye kuharibu ama kutishia kupotea kwa tunu hizo za Taifa, akiwataka kuangalia zaidi hatma zao na kung'ang'ana katika kuiacha Tanzania kuwa salama na iliyo bora zaidi.

No comments:

Post a Comment