VYAMA VYA UPINZANI VINATAKA KUVUNJA MUUNGANO WETU- CHILO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, October 24, 2025

VYAMA VYA UPINZANI VINATAKA KUVUNJA MUUNGANO WETU- CHILO



Aliyekuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano, Khamis Hamza Chilo amesema Chama Cha Mapinduzi kinaenda kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kutokana na sera zake za amani, utulivu na maendeleo tofauti na Sera za Vyama vingine vya Upinzani ambao sera zao zimekuwa za ubaguzi, maneno na kupinga maendeleo ya wananchi.

Chilo ametoa kauli hiyo wakati wa Kufunga Kampeni za Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja, Unguja Visiwani Zanzibar, akisema tayari wananchi wanafahamu kile ambacho CCM imefanya na kile ambacho wamepanga kukifanya kwa miaka mitano ijayo.

"Nimewasikia wapinzani wanasema hasa chama cha ACT Wazalendo, wanawaambia wananchi watakapopiga kura za mapema na wao waende kitu ambacho kinachochea ugomvi, kuleta uhasama, fujo na tafrani katika nchi yetu. Chama hiki pia kina ilani inayotekelezeka tofauti na Vyama vingine kwahiyo niwaombe sana twendeni tukakichague tena Chama Cha Mapinduzi.

"Vyama hivi vya upinzani vinapinga pia muungano, nimewasikia wanasema kipaumbele chao ni mamlaka kamili na ukiwasikiliza vyema unaelewa kuwa mamlaka kamili yao ni fujo na vurugu kwasababu mamlaka kamili tayari Zanzibar tunayo baada ya Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964." Ameongeza kusema Mhe. Chilo.

Chilo pia amemshukuru Dkt. Samia kwa kusimamia na kuulinda muungano wa Tanganyika na Zanzibar, akisema katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wake amesimamia uondoaji wa kero 15 za muungano na leo muungano umeendelea kuwa imara ikiwemo utoaji wa fedha nyingi kwa upande wa Zanzibar kutekeleza miradi ya maendeleo na miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

No comments:

Post a Comment