DKT. SAMIA AMETUPENDELEA VIJANA KWENYE UONGOZI WAKE- NG'WASI KAMANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 8, 2025

DKT. SAMIA AMETUPENDELEA VIJANA KWENYE UONGOZI WAKE- NG'WASI KAMANI


"Katika wakati wako uliotutumikia kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Vijana umetupendelea. Katika uwanja huu huu ulikuja ukazungumza na Vijana wa Tanzania katika uwanja huu na yote uliyoahidi umetekeleza kwa zaidi ya asilimia mia moja, tunakushukuru sana. Mhe. Rais Samia ulituahidi ajira na Chama Cha Mapinduzi wakati kinaomba ridhaa kilisema kitatoa ajira Milioni nane, ninavyozungumza mbele yenu leo nina furaha kuwaambia Mgombea mnayemuona mbele yenu ametekeleza kwa zaidi ya asilimia mia, ametoa ajira Milioni nane na elfu themanini na nne, mia mbili na tatu kwa kipindi cha miaka minne. Nani kama Dkt. Samia?

Hapa Mwanza katika Mikoa iliyonufaika ni sisi Vijana wa Mwanza, hapa kuna Ziwa Viktoria na kuna zaidi ya Vizimba 508 na boti zaidi ya 200, zote alikuja kuzikabidhi katika uwanja huu huu na Vijana wameuaga umaskini kupitia vizimba hivyo. Katika suala la elimu Vijana wote tunajua hali iliyokuwepo vyuoni kabla ya utawala wako na leo tunapozungumza hapa tunasoma kwa amani na tunakuahidi Vijana wote wa Vyuo na Vyuo vikuu ifikapo tarehe 29 Oktoba kura zote ni kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Wakati unaingia madarakani kwenye mifuko ya uwezeshaji wa vijana kiuchumi tulikuwa na shilingi Bilioni 945 tu inayozunguka kwa makundi yote ya Vijana, wanawake na wenye ulemavu. Leo hii mwaka 2025, mfuko huo unazungusha zaidi ya Trilioni 3.2.

"Unaowaona hapa ndugu mgombea wetu ni watu wa Mwanza, vitovu vyetu vimezikwa hapa na hata tukifa tutazikwa hapa, hatuwezi kuthubutu kufanya tendo lolote liwe kwa kudanganya, iwe kwa kushawishiwa kuharibu amani ya Mkoa huu na nchi hii kwasababu hatuna nchi nyingine, sisi na familia zetu kesho zetu zipo hapa. Ifikapo 29 Oktoba kazi pekee tunayotakiwa kuifanya kama Vijana ni kuhakikisha tunakuwa mabalozi wa amani, ni kuhakikisha tunawadhalilisha wale wote wenye nia hasi na chafu na nchi yetu, Vita hii ni ya kwetu na ni vita ya uzuri dhidi ya ubaya, ni ya amani dhidi ya machafuko na Vijana tutaipambana vilivyo."- Ng'asi Damas Kamani, Mbunge mteule wa Viti maalumu kundi la Vijana, akimnadi Mgombea wa nafasi ya Urais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Viwanja vya Nyamagana Mkoani Mwanza leo Jumatano Oktoba 08, 2025.


No comments:

Post a Comment