DKT. SAMIA KUENDELEA NA KAMPENI ZAKE KATORO, CHATO NA GEITA MJINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 13, 2025

DKT. SAMIA KUENDELEA NA KAMPENI ZAKE KATORO, CHATO NA GEITA MJINI



Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan Jumatatu ya leo Oktoba 13, 2025 anatarajiwa kuendelea na Kampeni zake Mkoani Geita, akitarajiwa kuomba kura na kunadi ilani ya Chama chake kwa wananchi wa maeneo ya Geita Mjini, Katoro, Nyawilimilwa na Wilayani Chato, ikiwa ni siku ya pili ya kampeni zake katika Mkoa huo.

Katika Miaka yake minne madarakani, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Mtangulizi wake Hayati Dkt. Samia Suluhu Hassan, Dkt. Samia kote alikopita kwenye Kampeni ameonesha matokeo makubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na utoaji na usimamizi wa huduma za kijamii na kiuchumi, simulizi za wanaoshuhudia matokeo hayo wakimtaja kama muarobaini ulioondoa mila kandamizi na imani haba na potofu kwa jamii, wengi wakionesha kutoamini ikiwa mwanamke angeliweza kufanya makubwa kama yaliyofanywa na Dkt. Samia ndani ya miaka minne pekee aliyowatumikia Watanzania.

Dkt. Samia anaingia Wilaya ya Geita leo Jumatatu, sehemu ambapo Ilani anayoinadi imeeleza mengi kama ahadi yake kuelekea mwaka 2030 ikiwemo Ujenzi wa soko la Samaki Katoro, ununuzi wa Boti moja ya uvuvi, Ujenzi wa barabara ya mzunguko (Round about) kufika maeneo ya Nyantorotoro Kibaoni, njia panda ya Nyankumbu- Nyang'hwale/Kakola, Njia panda ya Mbugani- Nendeni na Amani, Njia panda ya Mtakuja/Nyarugusu- Katoro kwa Lushanga na njia panda ya Mtunduni- Bugomola Mwanza na kwa Ngovongo pamoja na ujenzi wa masoko mawili ya mazao na maduka ya biashara (shoping mall) ya kisasa

Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2025/30 anayoinadi Dkt. Samia Suluhu Hassan pia imeahidi ujenzi wa barabara ya Kiwango cha lami ya kutoka Ushirombo kwenda Katoro (Km53), upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Nyankumbu- Nyang'hwale Jct - Wingi 3 - Nyang'holongo (Km149), Ujenzi wa Viwanda 4 vya kuchakata Alizeti Geita, Ujenzi wa machinjio 4 za kisasa, Ujenzi wa kituo cha biashara kwenye Mji wa Katoro, ujenzi wa majosho 11 kwaajili ya wafugaji wa Wilaya ya Geita pamoja na ujenzi wa Viwanja vinne vya kisasa kwaajili ya michezo mbalimbali Wilayani Geita.

No comments:

Post a Comment