DKT. SAMIA USIBABAISHWE NA CHOKO CHOKO ZA WACHACHE MTANDAONI- WASIRA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 9, 2025

DKT. SAMIA USIBABAISHWE NA CHOKO CHOKO ZA WACHACHE MTANDAONI- WASIRA



Akimtenganisha Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Stephen Wasira amemtaja Dkt. Samia kama kiongozi hodari na mzoefu katika Uongozi, akisema ametekeleza majukumu yake kwa muda mfupi na kwa mafanikio makubwa na kumsihi kutobabaishwa na kile alichokiita "Chokochoko za Mtandaoni".


Wasira ametoa kauli hiyo leo Oktoba 09, 2025 wakati wa Mkutano wa Kampeni za Dkt. Samia Bunda Mjini Mkoani Mara, akikumbusha namna ambavyo Dkt. Samia alivyoingia madarakani mwaka 2021 katika mazingira magumu na kutoeleweka sana na Watanzania kwa kile ambacho kingetokea mara baada ya Kifo cha Mtangulizi wake Hayati John Pombe Magufuli sambamba na uwepo wa janga alilolikuta la ugonjwa wa Korona.

"Wakati huo Dkt. Samia alituambia maneno mawili tu, Kazi iendelee na miaka minne baadaye kazi imeendelea na pamoja na mazingira yaliyokuwepo, Dkt. Samia ameongoza nchi yetu na kuhakikisha umoja na amani ya nchi yetu inaendelea kuwa na amani.

Zipo chokochoko nyingi na niwaambie chokochoko zile zipo kwa watu wachache wanaotumia mitandao ya kijamii. Naomba msome mitandao ile kwa uangalifu maana kuna watu wachache sana ambao hawaridhiki, kwa wale mnaopika maarage mnaelewa, kuna maarage huwa hayaivi, ukipika, yanabaki madogo yanaelea juu. Hao ndio wanaosumbua kwenye Mitandao na hao hawawezi kuisumbua nchi.

"Na nimwambie mgombea wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba wala asibabaishwe na watu hao wachache- hao wachache hata ukifanya vizuri namna gani watabaki kununa, hao wananunia mpaka mafanikio. Ipo bendi ya muziki hapa zamani iliwahi kusema tenda wema nenda zako, ninaamini watakukumbuka kwa wema wale wote wenye nia njema na bahati nzuri ndio wengi." Amesema Makamu Mwenyekiti huyo.

No comments:

Post a Comment