HAKI ZA WATANZANIA SASA HAZICHELEWI WALA KUPOTEA- DKT. SAMIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 22, 2025

HAKI ZA WATANZANIA SASA HAZICHELEWI WALA KUPOTEA- DKT. SAMIA



Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema sekta ya haki nchini Tanzania imeimarika katika kipindi cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya sita, akisema kuundwa kwa Tume mbalimbali za marekebisho kumesaidia katika maboresho hayo.

Dkt. Samia amebainisha hayo leo Jumatano Oktoba 22, 2025 wakati wa Mkutano wake wa Kampeni kwenye Viwanja vya Kecha, Kinyerezi, Wilayani Ilala Mkoani Dar Es Salaam akisema tofauti na miaka kadhaa iliyopita, sasa hivi haki za watanzania hazipotei na hakuna ucheleweshaji mkubwa wa Haki katika Vyombo vya Haki nchini Tanzania.

"Suala la utawala bora ni kuhakikisha unaongoza nchi na kuangalia masuala ya watu na kuwashirikisha watu wenyewe kwenye kuyapata masuala yanayowakera na kutoa suluhu ya masuala hayo na katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tuliunda Tume kadhaa za kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo Tume ya haki jinai kwenda kuangalia masuala ya haki jinai, haki za watu zinavyoamuliwa, zinapatikana vipi, wanabinywa vipi na mengineyo na tayari Tume ile ilimaliza kazi yake na ikatupa taarifa.

Sasa hivi sekta yetu ya haki, mahakama zetu, haki na sheria, ipo vizuri sana. Haki za watu sasa hazipotei kama zilivyokuwa, hazichelewi kama zilivyokuwa. Sasa hivi Polisi, Mahakama, Mpelelezi, Mwendesha Mashtaka, wote wanasomana na linaloandikwa leo Polisi, analisoma DPP, analisoma DCI, linasomwa mahakamani. Taarifa zote wanazotoa watu zinasomwa na vyombo vyote kwahiyo ule mchezo wa ndugu zetu kwenda kuweka maneno ya ziada kwenye maelezo ya mtu sasa hivi haipo, ulilolisema ndilo linalosomwa kote." Amesisitiza Dkt. Samia.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa ikiwa atapewa ridhaa ya kuunda serikali, ataendelea na ujenzi wa miundombinu ya sekta ya haki ikiwemo Mahakama za Wilayaz Mahakama za Mikoa na Mahakama Jumuishi ili kuendeleza kuboresha sekta hiyo ya haki nchini.

No comments:

Post a Comment