JAJI MKUU AKUTANA NA UONGOZI WA CMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 18, 2025

JAJI MKUU AKUTANA NA UONGOZI WA CMA


Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George M. Masaju, amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Mhe. Usekelege Mpulla, pamoja na Menejimenti ya Tume hiyo leo, Oktoba 17, 2025, jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Mahakama na CMA, pamoja na kubadilishana maoni na ushauri wa kuboresha huduma za utatuzi wa migogoro ya kazi.

Aidha, Mhe. Masaju ametoa wito kwa Tume kuendelea kuwajibika na kuwa wazalendo katika utendaji wa kazi, huku akisisitiza umuhimu wa kutoa haki kwa haraka na kwa usawa.

Viongozi wa Mahakama walioungana na Mhe. Jaji Mkuu katika kikao hicho ni pamoja na Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Abdi Kagomba, Kaimu Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Herbert, Mhe. Venance Mlingi, na Mhe. Clarence Mhoja.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Tume Mhe. Usekelege Mpulla, ameipongeza Mahakama kwa ushirikiano wake na kuahidi kuendelea kushirikiana katika kuboresha huduma za haki kazi nchini.


No comments:

Post a Comment