
Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) imewalipa Shilingi bilioni 1.6 wananchi 213 wa Kijiji cha Mpeta Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, wanaopisha utekelezaji wa mradi wa SGR kipande cha sita Tabora hadi Kigoma.
Hassan Mbaga ambaye ni mthamini na msimamizi wa zoezi la ulipaji fidia kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC ) amesema mradi wa SGR ni wa usanifu na ujenzi hivyo maeneo yanayohitajika kwa shughuli za mradi yamekuwa yakichukuliwa kwa hatua, hivyo kufanya zoezi la ulipaji fidia kuwa endelevu.
Hassan Mbaga ambaye ni ni mthamini na msimamizi wa zoezi la ulipaji fidia kutoka Shirirka la Reli Tanzania ( TRC ) amesema katika awamu ya pili ya ulipaji fidia katika kipande cha sita Tabora hadi Kigoma Serikali imelipa Shilingi bilioni 1.6 kwa wananchi 213 wa Kijiji cha Mpeta wilayani uvinza Mkoani Kigoma.

Akizungumzia zoezi hilo, Katibu Tarafa wa kata ya Nguruka, Wilaya ya Uvinza, Bwana Lyola Proches, ambaye katika zoezi la ulipaji fidia alimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mhe. Dinah Mathaman, alitoa wito kwa wananchi waliopokea fidia husika kuzitumia fedha walizopokea kwa umakini ambapo alisema, ‘’natoa rai kwenu kwamba fedha mlizopokea mkazifanyie malengo yaliyo sahihi hususani kurudisha vile vipande vilivyotwaliwa badala ya kufanya matumizo yasiyo na tija’’, alisisitiza Katibu Tarafa wa kata ya Nguruka, Wilaya ya Uvinza, Bw. Lyola Proches.
Wakati huo huo mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Mpeta Bw. Lifa Hamad Alpha, kwa niaba ya wenzake waliopokea fidia husika, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza ile ahadi waliyopewa kwenye fidia na kurudisha Maghala ya kuifadhia mpunga hivyo kuendelea na shughuli za kilimo.
Katika hatua nyingine, afisa Jamii kutoka Shirika la Reli TRC Lucy Maroda amesema Elimu waliyoitoa katika ulipaji Fidia itakwenda kuwasaidia wananchi hao ili kutimiza malengo yao na kufanya Uchumi wa wananchi kuimarika.
No comments:
Post a Comment