
"Uliniponipa dhamana ya kukusaidia katika eneo la maji tulipofika hapa Katavi hali ya upatikanaji wa maji hapa Mpanda ilikuwa asilimia 30, hali ya upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Katavi maeneo ya Vijijini ilikuwa asilimia 55. Katika kipindi cha miaka minne umetupatia Bilioni thelasini na tatu, Milioni mia tano ishirini na tisa, laki sita na thelasini na nne na mia tano ishirini na tisa kwaajili ya kutatua matatizo ya maji Mijini na Vijijini.
Katika eneo hili la Mjini tumetekeleza miradi mikubwa minne ikiwemo Mradi wa Ikolongo 2, Mradi wa Shankara, Mradi wa Kanoga na tumefanya ukarabati mkubwa wa miundombinu chakavu katika Mji huu wa Mpanda. Umeweza kututoa kwenye Asilimia 30 na hapa tunapozungumza leo tumefikia asilimia 68.7." Jumaa Aweso, Mgombea Ubunge Jimbo la Pangani, Tanga na Waziri wa Maji akimnadi Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi Oktoba 19, 2025 Mpanda Mjini kwenye Viwanja vya Azimio, Katavi.





No comments:
Post a Comment