JAMBO AMUOMBEA KURA DR. SAMIA SHINYANGA MJINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 18, 2025

JAMBO AMUOMBEA KURA DR. SAMIA SHINYANGA MJINI

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis akiwaombea kura wagombea (Diwani wa kata ya Mjini - Salum Kitumbo, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini - Patrobas Katambi na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan) kwenye mkutano wa Kampeni  Kata ya Mjini Jimbo la Shinyanga  Mjini  Ijumaa Oktoba 17,2025  

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Meatu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Salum Khamis maarufu Jambo,amemuombea kura nyingi za ushindi Mgombea Urais wa CCM Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi na Mgombea Udiwani Kata ya Mjini, Jimbo la Shinyanga Mjini Salum Kitumbo.

Jambo ameomba kura hizo leo Oktoba 17,2025, kwenye Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Udiwani wa Kata ya Mjini, Jimbo la Shinyanga Mjini Salum Kitumbo, uliofanyika viwanja vya Soko Kuu la Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na Mamia ya wananchi.

Amewaomba wananchi kwamba,siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 wajitokeze kwa wingi kupiga kura na wasifanye makosa, bali wakampigie kura nyingi za ushindi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Patrobas Katambi pamoja na Salum Kitumbo ili wapate kuwaletea maendeleo  kwa sababu ni viongozi makini na wenye kujali maslahi ya watu.

“Ndugu zangu wananchi wa Shinyanga Mjini, Oktoba 29 nendeni mkapige kura  kwa sababu ni haki yenu ya msingi na mkawachague wagombea wote wa CCM kuanzia ngazi ya Rais,Wabunge na Madiwani,”amesema Khamis.

Akimzungumzia Rais Samia,amesema ndani ya utawala wake wa miaka mitano amefanya mambo makubwa hapa nchini, pamoja na kuiletea maendeleo Kata ya Mjini,huku akimpongeza pia Patrobas Katambi, kwamba ni kiongozi mzuri ambaye ameaminiwa na Rais, na ameubadilisha mji wa Shinyanga, hivyo wanastahili kupewa mitano tena.

Amesema kwa upande wa Salum Kitumbo, amesema anamfahamu vizuri na kwamba Kata ya Shinyanga Mjini imepata Diwani ambaye ni mchapakazi, Mwaminifu, Mwadilifu na ambaye anajali maslahi ya watu sababu amefanya naye kazi siku nyingi na anamfahamu vizuri.
“Salum Kitumbo nasimama hapa kukuombea kura kwa wananchi wa kata ya Mjini,nina imani watakupatia ridhaa ya kuwa diwani wao,na kazi ya udiwani ni utumishi wa watu, nakuomba sana ukawatumikie wananchi,simu zipatikane na nyumbani kwako upatikane. kashughulikie matatizo ya wananchi na uwaletee maendeleo nafahamu utendaji wako kazi, sina mashaka na wewe”, amesema Khamis.

Naye Mgombea Udiwani Kata ya Mjini ,Salum Kitumbo,akimwaga sera kwa wananchi ameahidi kwamba atakamilisha ujenzi wa Soko Kuu la Mjini humo ili kuboresha mazingira rafiki kwa wafanyabiashara.

Ametoa ahadi nyingine kwamba barabara zote za mjini humo zitajengwa kwa kiwango cha lami katika mitaa yote, huku akiwaahidi pia kusimamia vyema suala la mikopo ya halmashauri asilimia 10 ili makundi husika ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu wapate kunufaika nayo na kuinuka kiuchumi.

TAZAMA PICHA👇👇

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis (kulia) akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Mjini Jimbo la Shinyanga  Mjini Salum Kitumbo. Picha zote na Kadama Malunde
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis (kulia) akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Mjini Jimbo la Shinyanga  Mjini Salum Kitumbo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni Kata ya Mjini - Shinyanga  Ijumaa Oktoba 17,2025
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis akiwaombea kura wagombea (Diwani wa kata ya Mjini - Salum Kitumbo, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini - Patrobas Katambi na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan)
Mgombea Udiwani Kata ya Mjini ,Salum Kitumbo akinadi sera 
Mgombea Udiwani Kata ya Mjini ,Salum Kitumbo akinadi sera 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis,akisalimiana na wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni Kata ya Mjini, Jimbo la Shinyanga Mjini
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis,akisalimiana na wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni Kata ya Mjini, Jimbo la Shinyanga Mjini
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis, akisalimiana na wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni.

No comments:

Post a Comment