
"Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuja na kauli mbiu ya Kazi na Utu na kazi anayoifanya Dkt. Samia ni kazi ya Utu. Zipo nadharia mtaani zinazosema Chama Cha Mapinduzi na Dkt. Samia hathamini watu, ukiangalia kazi anazozifanya zote zinagusa maisha ya Mtanzania kuanzia juu mpaka chini.
Utu wake ndiyo uliosababisha yeye kuja na Kampeni ya msaada wa kisheria kwa Watanzania nchi nzima, maana yake Mama Samia alimuona mtu wa chini kabisa asiyeweza kuwa na wakili kwasababu huko mtaani, huko Vijijini kuna akinamama wengi wanadhulumiwa mirathi yao, kuna wengi wanahangaika na ardhi na wapo wengi wanaoteseka na masuala ya kisheria. Lengo msaada huu wa kisheria umegusa wengi nchini.
"Kuna ndugu zangu Machinga wako Tanzania nzima, zamani walikuwa wanakimbizwa kama digidigi nchi nzima kwenye Miji, leo kwa kulielewa hilo amewasaidia machinga kila mahali wametengewa maeneo ya kufanya kazi na amewapa mikopo. Kama unajiona upo mbali, umetengwa, nikuambie Dkt. Samia anakuona huko ulipo." Mch. Peter Msigwa akimnadi Mgombea wa nafasi ya Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Alhamisi Oktoba 23, 2025 Wilayani Temeke Jijini Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment