NITAULINDA MUUNGANO WETUNKWA NGUVU ZANGU ZOTE- DKT. SAMIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, October 24, 2025

NITAULINDA MUUNGANO WETUNKWA NGUVU ZANGU ZOTE- DKT. SAMIA


Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaahidi wakazi wa Zanzibar na Tanzania bara kuwa ataendelea kuulinda Muungano wa nchi hizo mbili ikiwa atapewa ridhaa ya kuunda serikali, akisema Muungano huo umekuwa na faida kubwa kwa pande zote mbili.

Dkt. Samia ametoa ahadi hiyo leo Ijumaa Oktoba 24, 2025 wakati wa Mkutano wake wa Kampeni Visiwani Zanzibar kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Unguja, akiahidi pia kuimarisha na kufanyia kazi maendeleo Jumuishi kwa kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha huduma za kijamii zinamfikia kila mmoja ikiwemo huduma za maji na elimu pamoja na nishati ya umeme.

"Natambua kwasasa tuna changamoto kidogo ya umeme hapa Zanzibar lakini ndugu zangu nataka niwahakikishie mimi na Dkt. Mwinyi tumejipanga vyema kumaliza kadhia hii na muda si mrefu Zanzibar itakuwa na umeme wa uhakika kwa saa 24, siku saba za wiki." Amewahakikishia wananchi.

Dkt. Samia amezungumzia pia uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mitaji na fursa za biashara na kujiajiri, akiahisi kutia nguvu na bidii zaidi katika kuwawezesha Vijana kuweza kuajiriwa na kujiajiri ili kupata kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku.

Ameahidi pia kukuza uchumi mkubwa wa nchi, kwa kuimarisha vichocheo vya uchumi ikiwemo uimarishaji wa miundombinu ya usafiri na usafirishaji pamoja na kuhakikishia nishati ya umeme inakuwa ya uhakika pamoja na kusisimua sekta za uzalishaji ikiwemo sekta za Utalii, Uchumi wa buluu, Viwanda pamoja na sekta ya kilimo.

No comments:

Post a Comment