RAIS SAMIA NI MSIKIVU, AKIAHIDI ANATEKELEZA- AESHI HILALY - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, October 19, 2025

RAIS SAMIA NI MSIKIVU, AKIAHIDI ANATEKELEZA- AESHI HILALY



Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi Aeshi Hilaly amewaomba Wananchi wa Sumbawanga na Watanzania kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akimshukuru kwa usikivu wake na utekelezaji wa mahitaji ya wananchi wa Sumbawanga Mjini.

"Mhe. Mgombea wana Sumbawanga watakuwa mashahidi nikiwa bungeni kwa miaka kumi nimepambana kuomba uwanja wa ndege na mara ya mwisho niliomba bajeti ya uwanja wa ndege itolewe kwenye bajeti ya Bunge, lakini Mhe. Rais ulitusikiliza na tumepokea Bilioni 61, niombe kukuambia kuwa tumekamilisha uwanja ule kwa asilimia 90 na mimi ninaamini utautumia uwanja ule kusafiri kurudi nyumbani."

"La pili nilikuambia na kukuomba Mhe. Mgombea kuwa Sumbawanga tulikuwa na mradi wa maji wa shilingi Bilioni 52, mradi ule wakati tunaufanyia upembuzi yakinifu Sumbawanga haikuwa kubwa kama ilivyo leo kutokana na kukua kwake kwa kasi, nikakuomba Mama kuwa tuna mradi wa bwawa la maji ambalo linahitaji shilingi Bilioni 2. 500, Mama hukusita, palepale ukatoa maelezo na tayari tumepokea fedha hizo kujenga bwawa la maji na Bwawa hilo likikamilika Sumbawanga haitokuwa na shida ya maji mpaka mwaka 2040." Amesema Ndugu Aeshi.

Mgombea Ubunge huyo ametoa shukrani hizo na kuwaomba wananchi kumpa tena nafasi Dkt. Samia, wakati akizungumza na wananchi wa Sumbawanga kwenye Mkutano wa kampeni za Dkt. Samia kwenye Viwanja vya Kizwite, Sumbawanga Mjini Mkoani Rukwa leo Jumapili Oktoba 19, 2025, akimshukuru pia Dkt. Samia kwa mapinduzi makubwa kwenye sekta ya kilimo ikiwemo ongezeko kubwa la bei ya mahindi chini ya mfumo wa ununuzi wa mahindi kupitia Wakala wa hifadhi ya Taifa ya chakula NFRA.

Aeshi ameeleza kuwa bei ya mahindi imepanda mara mbili chini ya Miaka minne ya serikali ya awamu ya sita ikianzia shilingi 650 na baadaye kuwa shilingi 700 kwa kilo suala ambalo limeondoa kilio cha wananchi na wakulima wa Sumbawanga waliokuwa wakiuza gunia la mahindi kwa shilingi 30,000.

Amezungumzia pia suala la afya ndani ya Jimbo la Sumbawanga Mjini akisema wakati Dkt. Samia anaingia madarakani mwaka 2021 Jimbo hilo lilikuwa na kituo kimoja cha afya na leo vipo vituo nane vya afya, akisisitiza wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwani yajayo ni mazuri zaidi katika kustawisha ustawi wa jamii.


No comments:

Post a Comment