"Ndugu zangu wananchi wa Rukwa leo tarehe 19 mwezi wa kumi tunahesabu tumebakiwa na siku kumi kabla ya uchaguzi Mkuu, sasa ule wakati ambao wananchi wote tumeusubiri kwa hamu ili tufanye maamuzi kuhusu Viongozi tunaowataka unakaribia kufika.
Na wale waliokuwa wanasema mwezi wa kumi tuna jambo letu, Jambo linakaribia kufika na ni siku kumi tu zijazo, hivyo inabidi kila mmoja wetu ajiandae, kila mtu aangalie kadi yake ya kupiga kura ilipo aiweke vizuri na kwakuwa siku hiyo ni siku ya mapumziko sote hatuna budi kuhimizana na kuhamasishana kutoka mapema ili tukatumie haki yetu ya kikatiba ua kupiga kura."- Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM akizungumza na wananchi wa Sumbawanga Mjini leo Jumapili Oktoba 19, 2025.


No comments:
Post a Comment