Na OKULY JULIUS, OKULY BLOG, DODOMA
Serikali imesisitiza dhamira yake ya kuibadilisha sekta ya elimu ili iendane na mahitaji ya uchumi wa dunia unaobadilika kwa kasi na unaoendeshwa na teknolojia, huku ikihakikisha elimu jumuishi, yenye usawa na ubora kwa wote.
Akizungumza leo Oktoba 22,2025 jijini Dodoma wakati akifungua wa Mkutano wa Pamoja wa Mapitio ya Sekta ya Elimu (AJESR) wa mwaka 2024/25, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Daniel Mushi, alisema serikali imejipanga kuhakikisha mfumo wa elimu unaendana na mikakati ya maendeleo ya taifa, ikiwemo ajenda ya uendelezaji wa viwanda na ubunifu chini ya Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050.
“Huu ni miongoni mwa mikutano muhimu zaidi katika mfumo wetu wa elimu kwani unatoa jukwaa rasmi la majadiliano ya sekta nzima, uwajibikaji wa pamoja na kupanga kwa kuzingatia ushahidi,” amesema Prof. Mushi.
AJESR yenye kaulimbiu “Kubadilisha Elimu kwa Maendeleo Endelevu,” inawakutanisha wadau kutoka taasisi za serikali, washirika wa maendeleo, asasi za kiraia, taasisi za dini na sekta binafsi ili kupitia utekelezaji wa sekta ya elimu, kutambua changamoto na kukubaliana juu ya vipaumbele na hatua za kuchukua kwa mwaka unaofuata.
Profesa Mushi alisema serikali inaendelea kuangalia elimu kama uwekezaji katika rasilimali watu, na si huduma ya kijamii pekee, akibainisha kuwa nchi inajenga nguvu kazi yenye ujuzi na weledi wa kuendesha ubunifu na tija.
“Dunia inabadilika kwa kasi sana, teknolojia inachukua nafasi kubwa, hivyo tunahitaji rasilimali watu waliobobea watakaoweza kwenda sambamba na maendeleo hayo ya kiteknolojia,” alisisitiza.
Amewapongeza wadau wa elimu kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mwaka 2024/25, ikiwemo kuongezeka kwa upatikanaji wa elimu, kuboreshwa kwa mafunzo kwa walimu, mageuzi ya mitaala, na mifumo bora ya tathmini ya wanafunzi.
Prof. Mushi ameongeza kuwa kupitia AJESR, Tanzania inaendelea kuimarisha ushirikiano ambao umechangia kuunganisha sayansi, teknolojia na ubunifu katika mfumo wa elimu, hatua inayoiweka nchi katika nafasi nzuri ya kukabiliana na mahitaji ya uchumi wa karne ya 21.
“Maendeleo tuliyopata katika sekta ya elimu yanatokana na ushirikiano thabiti wa kiufundi na kifedha tulioujenga kwa miaka mingi,” amesema Prof. Mushi.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia elimu, Bw. Atupele
Mwambene, alisema elimu ni nguzo kuu ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2050 na msingi wa maendeleo ya rasilimali watu nchini.
“Rasilimali watu ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa lolote.
Ukuaji wa uchumi unaotegemewa unatokana na maandalizi bora ya rasilimali watu,” alisema, huku akihakikisha kuwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI itaendelea kusaidia shule katika kutekeleza mageuzi ya elimu ipasavyo.

Kwa niaba ya washirika wa maendeleo, Bi. Godfrida Magubo, Mkuu wa Ofisi ya Tume ya Uingereza nchini Tanzania, aliipongeza serikali kwa kipaumbele inachokipa elimu chini ya Dira ya 2050, akisisitiza kuwa bila kuwa na wananchi walioelimika vizuri, ukuaji jumuishi hautowezekana.
Bi. Magubo ameishauri serikali kuharakisha maandalizi kwa ajili ya mwaka 2027, ambapo takribani wanafunzi milioni 5.1 wataingia katika shule za sekondari za chini kutokana na kupunguzwa kwa muda wa elimu ya msingi kutoka miaka saba hadi sita.
Amesisitiza haja ya kuongeza madarasa, walimu na vifaa vya kujifunzia, na akashauri serikali kushirikiana na sekta binafsi pamoja na taasisi za dini ili kupata rasilimali zaidi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Simon Nanyaro, ameipongeza serikali kwa kuwekeza katika mafunzo ya walimu, akibainisha kuwa walimu 70,657 wa shule za msingi na 67,254 wa sekondari wamepatiwa mafunzo, ongezeko kubwa ikilinganishwa na walimu 1,250 waliokuwa wamefunzwa hapo awali.
“Tunapopitia utendaji wa elimu kwa mwaka 2024/25, tunasherehekea mafanikio na kupanga njia ya kwenda mbele. Tuitumie hekima na utaalamu wetu wa pamoja kuinua zaidi ubora na usawa wa elimu nchini,” alisema Bw. Nanyaro.

No comments:
Post a Comment