
Shirika la Special Olympics Tanzania leo Oktoba 21, 2024 limeendesha mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari za michezo kutoka vyombo mbalimbali nchini, yakilenga kuongeza uelewa kuhusu namna bora ya kuripoti na kuhabarisha jamii juu ya vipaji vya watu wenye ulemavu wa akili kupitia michezo.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa uwanja wa Benjamin William Mkapa jijini Dar es Salaam mafunzo yameendeshwa na Mr. Charles Rays Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Special Olympics Tanzania na yamekusudia kujenga ushirikiano imara kati ya vyombo vya habari na Special Olympics Tanzania, ili kuhakikisha simulizi chanya kuhusu uwezo na mafanikio ya watu wenye ulemavu wa akili zinapata nafasi kubwa zaidi katika vyombo vya habari.

Mafunzo haya ni sehemu ya mpango endelevu wa Special Olympics Tanzania wa kuimarisha ushirikiano na wadau wa habari ili kuendeleza ajenda ya ujumuishaji na fursa sawa katika sekta ya michezo kwa watu wote.



No comments:
Post a Comment