
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya na Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Amollo Odinga, amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo, Jumanne tarehe 14 Oktoba 2025, nchini India alipokuwa akipokea matibabu.
Taarifa kutoka kwa familia ya Odinga zimethibitisha kifo hicho, zikieleza kuwa kiongozi huyo mkongwe alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Raila, ambaye pia alikuwa kiongozi wa upinzani kwa muda mrefu nchini Kenya, alihusishwa pakubwa katika harakati za mageuzi ya kisiasa na demokrasia tangu enzi za mfumo wa chama kimoja.
Mpaka sasa, viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Kenya wameanza kutuma salamu za rambirambi kwa familia, chama cha ODM, na wananchi wa Kenya kwa jumla.
Mipango ya mazishi inatarajiwa kutangazwa na familia katika siku chache zijazo.
No comments:
Post a Comment