
Ndani ya Miaka minne ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, mambo mengi yamefanyika. Eneo moja muhimu ambalo limewagusa wengi ni katika uboreshaji wa maisha ya watu na ustawi wa Jamii ya Kitanzania ikiwemo kuendelea kutoa elimu bila ada kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita ambapo katika kipindi cha 2020- 2024 jumla ya shilingi 1, 308, 900, 040, 500 zimetumika kugharamia sera hiyo na hivyo kubakiza fedha nyingi mikononi mwa wazazi na walezi wanaosemesha watoto.
Hatua hii kulingana na Chama Cha Mapinduzi CCM chini ya Dkt. Samia ambaye pia ni Mgombea Urais kwenye uchaguzi Mkuu ww Oktoba 29, 2025 imewezesha kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza kutoka wanafunzi 722, 893 mwaka 2020 hadi kufikia wanafunzi 1, 056, 789 mwaka 2024 na kidato cha tano kutoka wanafunzi 78, 434 hadi wanafunzi 127, 008, hali iliyochochea kuongezeka pia kwa kiwango cha wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari kufikia asilimia 70.
"Tumewarejesha pia kwenye masomo wanafunzi wa kike 10, 864 katika shule za msingi na sekondari ili kuendelea na masomo. Tumeongeza pia idadi ya wanafunzi wanaojiunga elimu ya juu kutoka wanafunzi 233, 734 mwaka 2020 hadi wanafunzi 334, 854 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 43.3" imesema Ilani ya 2025/30.
Kadhalika ndani ya Miaka minne ya serikali ya awamu ya sita kumeongezeka kiwango cha ufaulu katika mitihani ya ngazi mbalimbali za elimu, ikiwemo ufaulu wa darasa la saba kufikia asilimia 80.6 mwaka 2023, Kidato cha nne kutoka asilimia 85.8 mwaka 2020 hadi 89.37 mwaka 2024 na kidato cha sita kutoka 89.37% hadi kufikia ufaulu wa 99.% mwaka 2024.
Aidha Serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata mikopo ya elimu ya juu kutoka wanafunzi 142, 170 mwaka 2020 hadi wanafunzi 245, 799 mwaka 2024, zikituma jumla ya shilingi trilioni 2. 760 kwaajili ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
"Tumeanza pia kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada ambapo wanafunzi 9, 959 wamenufaika katika fani za kipaumbele ikiwemo afya, kilimo, usafirishaji, ualimu wa ufundi na ufundi stadi na uhandisi wa nishati na madini." Sehemu ya Ilani imesema.
Serikali ya awamu ya sita pia imeanzisha Samia Scholarship ambapo wanafunzi 3, 696 wamenufaika kufikia mwaka 2024, serikali pia ikihuisha sera ya Taifa ya elimu na mafunzo pamoja na mitaala yake ili kuwezesha kutoa wahitimu mahiri na wanaokidhi mahitaji ya soko la ajira.
No comments:
Post a Comment