TUMEDHAMIRIA KUENDELEA KUINUA WAKULIMA NA WAFUGAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 20, 2025

TUMEDHAMIRIA KUENDELEA KUINUA WAKULIMA NA WAFUGAJI



Mgombea wa Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea kutoa ruzuku za mbolea, pembejeo za kilimo na ruzuku za chanjo kwa Mifugo ikiwa atachaguliwa kuunda serikali katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Dkt. Samia ametoa ahadi hiyo leo Jumatatu Oktoba 20, 2025 akiwa Wilayani Kibiti Mkoani Pwani kwenye muendelezo wa kampeni zake za uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akisema ruzuku hizo zimesaidia kuongeza uzalishaji wa mazai ya kilimo pamoja na kutoa soko la uhakika la kimataifa kwa wanyama hai na mazao ya mifugo ikiwemo nyama na ngozi.

"Hii maana yake ni kuwa tulipotoa pembejeo kwa ruzuku ina maana kuna fedha tuliiacha Mkononi kwako na tunapotafuta masoko na bei inapokuwa nzuri maana yake tunaingiza fedha mfukoni mwako, hii maana yake tumemuwezesha mkulima kurejesha jasho lake na kuendesha maisha yake na hii ndiyo kumuwezesha mwananchi kiuchumi."ameongeza Dkt. Samia.

Amezungumzia uzalishaji wa Korosho Wilayani humo akisema uzalishaji umeongezeka kutoka Kilogramu Milioni Mbili na laki nane na tisini hadi kufikia Kilogramu Milioni tisa huku pia ufuta uzalishaji wake ukiongezeka kutoka Kilogramu Milioni tano na laki tatu hadi Kilogramu Milioni kumi na moja.

Katika upande wa mifugo, Dkt. Samia mbali ya kuahidi kuendelea na kampeni ya chanjo na utambuzi wa mifugo, amewahakikishia wafugaji kuwa Tanzania imepata soko la uhakika la Kimataifa la mifugo na bidhaa zake, akisisitiza kuendelea zaidi kuinua sekta hiyo ikiwa atapewa nafasi ya kuunda serikali kupitia uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

No comments:

Post a Comment