TUTANUNUA BOTI 10 ZA UVUVI KIBITI- DKT. SAMIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 20, 2025

TUTANUNUA BOTI 10 ZA UVUVI KIBITI- DKT. SAMIA


Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hasssan leo Jumatatu Oktoba 20, 2025 akiwa Kibiti Mkoani Pwani, ameahidi ununuzi wa Boti kumi za uvuvi Wilayani humo ili kuongeza uzalishaji wa samaki.

Dkt. Samia ametoa ahadi hiyo leo wakati wa muendelezo wa Kampeni zake za uchaguzi Mkuu wa Tanzania, akisema ununuzi wa boti hizo pamoja na Vifaa vingine vya uvuvi ni muendelezo wa uwezeshaji wananchi katika sekta ya Uvuvi, akisema Boti nyingine kumi zilizotolewa katika Miaka yake minne ya Uongozi zimeongeza uvunaji wa samaki kutoka Kilogramu 650,000 hadi Kilogramu 4,600,000 za samaki.

Akizungumzia mafanikio ya sekta za Kijamii yaliyopatikana kwenye sekta ya afya Wilayani Kibiti, Dkt. Samia amesema kwa miaka minne ya serikali ya awamu ya sita wameongeza upatikanaji wa vifaa tiba na dawa kutoka asilimia 46 hadi asilimia 87 suala ambalo limeondoa kilio cha wananchi wengi kukosa dawa kwenye Vituo vya afya sambamba na kuhakikisha kuwa Vituo vyote vya afya vinakuwa na vipimo muhimu ili kuondoa adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata vipimo.

Vilevile Serikali ya awamu ya sita imeboresha Hospitali ya Wilaya na Kuongeza jengo la dharura, Jengo la kuhudumia wagonjwa mahututi na ujenzi wa wodi mbili za upasuaji kwenye Hospitali ya Wilaya, ikipunguza pia adha ya kufuata huduma za matibabu nje ya Wilaya ya Kibiti.

No comments:

Post a Comment