TUMEKUZA FURAHA NA UHURU KWA WATANZANIA- DKT. SAMIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 23, 2025

TUMEKUZA FURAHA NA UHURU KWA WATANZANIA- DKT. SAMIA


Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika eneo la furaha na Uhuru kwa Watanzania, serikali yake ya awamu ya sita imefanya vizuri, akiahidi kuendelea kutia bidii zaidi katika kuwafanya Watanzania kuwa na uhuru na furaha.

Dkt. Samia ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Oktoba 23, 2025 wakati wa Mkutano wake wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwenye Viwanja vya Tanesco Buza, Wilayani Temeke Mkoani Dar Es Salaam, akisema Uhuru wa watu kutoa maoni, kujumuika na uhuru mwingine usioenda kinyume na mila na tamaduni za Mtanzania umeimarika katika Miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita, ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa maendeleo jumuishi kwa kila mmoja ikiwemo uzingatiaji wa watu wenye mahitaji maalumu nchini.

"Kama unakaa pazuri, unakula vizuri, afya nzuri, maji unayapata, umeme unauona, unapopata kuwasha tv unawasha maana yake furaha ipo tu, ukitaka haki yako unaipata, michezo unacheza kwahiyo kwa eneo la furaha tumefanya vizuri na tunajipanga kufanya vizuri zaidi." Amesema Dkt. Samia.

Amezungumzia pia namna ambavyo sekta ya michezo na muziki imeimarika suala ambalo limekuwa likiwapa fedha na kukuza burudani kwa watanzania huku pia walemavu mbalimbali ikiwemo walemavu wa ngozi wakijumuishwa katika maendeleo pamoja na kuhakikishiwa uhuru na usalama dhidi ya dhana mbalimbali ikiwemo mauaji na uvamizi uliokuwa ukifanywa kwa walemavu wa ngozi kwa kuamini kuwa Viungo vyao vinaweza kuleta utajiri.

No comments:

Post a Comment