TUTAMALIZA CHANGAMOTO YA MAFURIKO BONDE LA RUFIJI- DKT. SAMIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 20, 2025

TUTAMALIZA CHANGAMOTO YA MAFURIKO BONDE LA RUFIJI- DKT. SAMIA


Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa ikiwa atapewa ridhaa ya kuunda serikali, kwa Wilaya ya Rufiji wanatarajia kujenga Miradi miwili ya umwagiliaji na Skimu ya umwagiliaji ya Hekta 13,000 kwenye Bonde la Mto Rufiji ili kusisimua kilimo cha umwagiliaji na uthibiti wa mafuriko.

Dkt. Samia ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Oktoba 20, 2025 wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Rufiji kwenye Viwanja vya Ujamaa Ikwiriri kwenye Mkutano wake wa Kampeni akisisitiza kuwa tayaro Mkandarasi amepatikana na takribani shilingi Bilioni 245 zitatumika.

Katika mradi huo, Dkt. Samia amesema utahusisha pia ujenzi wa zuio la mafuriko kwenye Wilaya hiyo pamoja na ujenzi wa barabara ya zaidi ya Kilomita 90 kwa kiwango cha lami pamoja na Makalavati ili kusaidia udhibiti wa maji ya mvua kwenye misimu ya Mvua, akisema mradi huo utamaliza kabisa changamoto ya Mafuriko katika Wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment