TUPENI KURA TUKAHESHIMISHE UTU WENU- DKT. SAMIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 20, 2025

TUPENI KURA TUKAHESHIMISHE UTU WENU- DKT. SAMIA


"Chama Cha Mapinduzi kazi yetu kufanya kazi kujenha utu wa mtu. Niliyoyaeleza yote huduma za kijamii, uwezeshaji wananchi kiuchumi na hii miradi ya kukuza uchumi mkubwa yote ni kujenga utu wa mtu na kuheshimisha utu wa mtu. Unapopata chakula cha kutosha, una afya ya kutosha na unapougua hospitali zipo, mtoto anaenda shule unamuona na haulipi, umeme upo nyumbani unakusaidia badala ya kukuna nazi siku hizi unakuna kwa blenda, mnakatakata mnasaga lakini pia chakula cha kutosha kipo nyumbani, umeuza pesa ipo na nyumba sasa zimeboreshwa zimekuwa za lami, huko ni kujenga utu wa Mtu.

 Niwaombe, tumekuja kuwaomba kazi, mtupe kazi tukajenge utu wa Mtanzania na kazi tunayoiomba tumeiweka kwenye Vijitabu vidogo vya Ilani na zipo kazi tutakazozifanya ndani ya Jimbo hili la Rufiji na Mkoa mzima wa Rufiji. Kwahiyo tunaowaomba kura mkichague Chama Cha Mapinduzi ili tukaifanye kazi tuwaletee maendeleo na tulinde, kunawirisha na kuheshimisha utu wenu."- Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea wa nafasi ya Urais wa Tanzania akiomba kura kwa wananchi wa Rufiji Mkoani Pwani leo Jumatatu Oktoba 20, 2025 kwenye Viwanja vya Ujamaa Ikwiriri.

No comments:

Post a Comment