WAZIRI MKUU APONGEZA WIZARA YA NISHATI KWA USIMAMIZI THABITI WA MIRADI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 16, 2025

WAZIRI MKUU APONGEZA WIZARA YA NISHATI KWA USIMAMIZI THABITI WA MIRADI




Na Mwandishi Wetu, Tanga


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amepongeza Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa utekelezaji na usimamizi miradi mbalimbali ya nishati nchini.

Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo jijini Tanga wakati akifunga Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula ya Duniani ambayo leo yamefikia kilele chake.

Mhe. Majaliwa amesema kuwa usimamizi mzuri wa miradi ya Nishati umepelekea wananchi kuendelea kupata huduma bora.

Katika maadhimisho hayo ya Siku ya Chakula Duniani yaliyoanza tarehe 10 Oktoba 2025 yamepelekea wananchi kupata elimu kuhusu mafanikio ya sekta ya nishati na miradi inayoendelea huku wananchi 500 wakinufaika na mitungi ya gesi iliyokuwa ikiuzwa kwa bei ya Ruzuku ya shilingi 17,500/=.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekabidhi tuzo kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni kupongeza juhudi za taasisi hiyo kupitia maadhimisho hayo ya Siku ya Chakula Duniani.






No comments:

Post a Comment