Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, ambaye pia ni Mlezi wa Kata ya Kandawe – CCM, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax, tarehe 26 Oktoba 2025 amehitimisha Kampeni za udiwani Kata ya Kandawe Wilaya Magu, Mkoa wa Mwanza, na kumnadi Mgombea udiwani wa Kata hiyo Komredi Lucas Bomoa na kuwaombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Magu ndugu Boniventure Kiswaga, na Mgombe wa nafasi ya Rais kupitia Chama cha Mapinduzi – CCM, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akiwanadi Wagombe wa CCM, Waziri Tax, amewakumbusha wana Kandawe na Watanzania kwa ujumla kujivunia maendeleo yaliyopatikana chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwemo Maji, Umeme, Ujenzi wa Miundombinu kama vile Barabara na madaraja, Shule, Hispitali na Vituo vya Afya nchini kote, ikiwemo Kata ya Kandawe.
Amewaomba kukichagua Chama cha Mapinduzi katika nafasi ya Rais, Mbunge na Diwani ili kiweze kuendeleza maendeleo na kupata maendeleo zaidi kuputia Miradi iliyoanishwa katika Ilani ya CCM ya 2025 - 2030.
Aidha, kupitia Mkutano huo wa kuhitimisha Kampeni katiki ya Kata ya Kandawe, Wilani Magu Mwanza, Mhe. Dkt. Tax, amewatoa hofu Watanzania na kuwataka kutokuwa na wasiwasi kuhusu hali ya Ulinzi na Usalama nchini kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 2025, kwani chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimeendelea kuimarika, na vipo makini, macho, imara, madhubuti na tayari kulinda usalama wa raia na mali zao wakati wote, na kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa amani.
Naye, Mgombea udiwani ndugu Lucas Bomoa, amewaomba wana Kandawe kumpa nafasi nyingine katika Uchaguzi wa tarehe
29 Oktoba 2025 ili aendeleze utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea na mipya kama iliyoainishwa katika ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Aidha, Mgombea huyo wa Udiwani amemshukuru Mlezi wa Kata ya Kandawe ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na JKT, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, kwa ulezi wake mahiri, na kujitoa kwa hali na mali katika kukijenga na kukiimarisha Chama katika maeneo mbalmbali ya Jimbo la Magu ikiwemo Kata ya Kandawe.

No comments:
Post a Comment