DKT. MWIGULU KUFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA USAFIRI ENDELEVU ARDHINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 26, 2025

DKT. MWIGULU KUFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA USAFIRI ENDELEVU ARDHINI



Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 26, 2025 anafungua Maadhimisho ya Wiki ya Usafiri Endelevu Ardhini Mwaka 2025 yanayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Malengo ya maadhimisho hayo ni pamoja na kuimarisha usalama na ufikivu wa huduma za usafiri wa nchi kavu kwa kukuza mifumo salama, jumuishi na endelevu ya usafiri wa ardhini kwa njia ya barabara na reli

Pia, yanalenga kukuza ushindani wa haki na ubora wa huduma katika usafiri wa nchi kavu kwa kuhakikisha waendeshaji wanatoa huduma za bei nafuu, zenye uhakika na ubunifu chini ya mfumo madhubuti wa udhibiti wa LATRA.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Nishati Safi na Ubunifukatika Usafirishaji.


No comments:

Post a Comment