MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO TARURA AHITIMU SHAHADA YA UMAHIRI YA SANAA KATIKA MAWASILIANO KWA UMMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 27, 2025

MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO TARURA AHITIMU SHAHADA YA UMAHIRI YA SANAA KATIKA MAWASILIANO KWA UMMA




Na Mwandishi Wetu, Kibaha,Pwani


Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa TARURA Bi. Catherine Sungura leo tarehe 27/11/2025 amehitimu Shahada ya Umahiri ya Sanaa katika Mawasiliano kwa Umma katika Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) katika mahafali ya 44 yaliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani.

Akiongea na waandishi wa habari Bi. Sungura amesema kwamba Shahada hiyo ni hatua inayotarajiwa kuongeza weledi katika usimamizi wa taarifa za taasisi, kuimarisha utoaji wa taarifa kwa wananchi pamoja na kuendeleza ushirikiano na wadau ili kuboresha taswira ya TARURA katika utekelezaji wa majukumu yake nchini.

No comments:

Post a Comment