
Kiungo wa kati wa England Kobbie Mainoo anakaribia kuondoka Manchester United kuelekea Napoli huku juhudi za kufikia mkataba wa bila malipo kwa mchezaji huyo wa miaka 20 zikiongezwa. (Teamtalk)

Barcelona itamsijili Marcus Rashford kutoka Manchester United kwa mkataba wakudumu endapo mchezaji huyo wa kimataifa wa England atakubali pendekezo lao la mshahara. (Talksport)

Wakala Niclas Fullkrug anasema ''heri'' mshambuliaji huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32 aondoke klabu ya West Ham. (TOMorrow Business Podcast via Athletic)

Mlinzi wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 24, amesema ''alikamia'' sana kujiunga na Real Madrid kabla ya kusaini mkataba mpya na The Gunners mwezi Septemba. (Sports Illustrated)

Idara ya usajili ya Newcastle imemtaja kiungo wa Atalanta Ederson, 24, katika mikutano ya hivi majuzi kama mrithi anayepigiwa upatu kuchukua nafasi ya Mbrazil mwenzake Joelinton, 29. (The I)

Liverpool wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa River Plate mwenye umri wa miaka 18 kutoka Argentina Ian Subiabre. (Fichajes - kwa Kihispania)

No comments:
Post a Comment