TETESI ZA SOKA ULAYA : REAL MADRID WAPO TAYARI KUMUUZA VINICIUS Jr. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 5, 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA : REAL MADRID WAPO TAYARI KUMUUZA VINICIUS Jr.


Real Madrid imeamua kumuuza mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr, 25, mwenye umri wa miaka 25 msimu ujao kufuatia mwenendo wake alipotolewa uwanjani wakati wa mechi yao na Barcelona. (Bild - kwa Kijerumani)

Mshambuliaji wa Brazil Rodrygo anataka kuondoka Real Madrid mwezi Januari, huku Arsenal na Tottenham zikimuwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Fichajes - kwa Kihispania)

Manchester United iko tayari kumwachia winga wa Uingereza Jadon Sancho, 25, ambaye anachezea klabu ya Aston Villa kwa mkopo, kuondoka kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Sportsport)

Klabu ya Roma inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uholanzi Joshua Zirkzee mwezi Januari. (Calcio Mercato - kwa Kiitaliano)

Beki wa Inter Milan na Ujerumani Yann Bisseck, 24, anatamani kuhamia Uingereza, huku West Ham na Tottenham zikitarajiwa kuwa makao yake mapya. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Crystal Palace, Inter Milan na Juventus watachuana kuwania saini ya beki wa Manchester City na Uholanzi Nathan Ake, 30 Januari. (Caught offside)

Manchester United inatarajiwa kuongeza juhudi katika mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Nottingham Forest ya Uingereza Elliot Anderson mwezi Januari, huku Mashetani Wekundu wakiamini kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 "anatamani sana" kuhamia Old Trafford. (Teamtalk)

Beki wa timu ya taifa ya Uholanzi Virgil van Dijk aliingiwa na wazo la kuhamia Real Madrid msimu uliopita kabla ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kusaini mkataba mpya na Liverpool (AS - kwa Kihispania)

Everton haitamuuza beki wa Uingereza Jarrad Branthwaite ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 70, licha ya Manchester United kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Teamtalk)

Meneja wa zamani wa Manchester United Erik ten Hag ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuwa kocha anayefuata wa Wolves. (ESPN)

No comments:

Post a Comment