Katika mchezo wa fainali, TFS Wino walitwaa ubingwa baada ya kuifunga Magingo FC kwa mikwaju ya penalti, kufuatia sare tasa ndani ya dakika 90.
Akizungumza wakati wa hitimisho la bonanza hilo Jana Novemba 25,2025, Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Kapenjama, alisema mashindano hayo ni zaidi ya burudani kwa kuwa yanatumika kutoa elimu muhimu ya uhifadhi.
Alisema misitu ni mhimili wa uchumi wa kijani, akawataka wananchi kuachana na matumizi ya moto kwenye maandalizi ya mashamba hususan msimu huu wa kilimo, kwani husababisha uharibifu wa rasilimali na mazingira.
Kwa upande wake, Mhifadhi Muandamizi wa Shamba la Miti Wino, Glory Kasmir, alisema bonanza hilo ni njia shirikishi ya kuwaunganisha wananchi na TFS kupitia elimu ya ulinzi wa misitu, mbinu salama za maandalizi ya mashamba na udhibiti wa moto misituni, sambamba na kuinua vipaji vya michezo kwa vijana.
Baadhi ya wakazi na washiriki wa mashindano hayo walisema elimu waliyoipata itawasaidia kuimarika kiuchumi kupitia kilimo salama na shughuli rafiki kwa mazingira, huku wakiahidi kuwa mabalozi wa uhifadhi katika vijiji vyao kwa kutekeleza mafunzo ya TFS katika maisha ya kila siku.
















No comments:
Post a Comment