TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 11, 2025

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA



Na Sixmund Begashe, Arusha


Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini (M&E) kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza ukusanyaji wa taarifa na takwimu kwa ajili ya tathmini ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Wizara (2021/2022–2025/2026) katika mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro.

Akizungumza kuhusu ziara hiyo inayoongozwa na Mtaalamu Mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof. Francis Mwaijande, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Ufuatiliaji wa Wizara, Mchumi Mkuu, Albert Dede amesema kuwa ukusanyaji wa taarifa unahusisha idara na vitengo vya Wizara, taasisi zake, wadau wa maendeleo, sekta binafsi pamoja na jumuiya za kijamii.

“Lengo ni kusaidia Wizara kutambua mafanikio, changamoto, na maeneo yanayohitaji maboresho. Tathmini hii itakuwa msingi wa maandalizi ya Mpango Mkakati mpya wa Wizara kwa kipindi cha 2026/2027–2030/2031,” amesema Dede.

Ameongeza kuwa zoezi hilo limeanza vizuri kwa timu hiyo kukutana na kukusanya taarifa kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) mkoani Arusha, pamoja na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Burunge mkoani Manyara.

Kwa upande wake, Afisa Utalii wa Hifadhi ya Wanyamapori Burunge, William Ruta, ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuanzisha zoezi hilo, akibainisha kuwa litachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha maendeleo ya jumuiya hiyo na jamii kwa ujumla.


No comments:

Post a Comment