Serikali inaendelea kuhakikisha ujenzi wa mabwawa ya takasumu unafanyika kwa viwango na kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji, pamoja na usalama.
Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Maji, Wizara ya Maji Bwn. Heri Chisute amesema katika mkutano wa mwaka unaohusu usalama wa mabwawa.
Amesema uhakika wa usalama, utii, na ulinzi wa mazingira si kwa kuangalia sheria pekee bali pia ni wajibu wa maadili kwa jamii zinazotegemea mifumo hiyo kwa ustawi wao ili kuepuka changamoto zinazoweza kutokea kwasababu ya mabwawa hayo.
Amesema hadi hivi sasa kuna idadi ya jumla ya mabwawa ya maji zaidi ya 700 na mabwawa ya taka sumu yakiwa zaidi ya 60.
Mkutano huo umewakutanisha watalaamu mbalimbali kutoka Sekta ya Umma na Binafsi,sambamba na kauli mbiu “Tahadhari za dharura za kukabiliana na Majanga ya mabwawa ya maji na topesumu”






No comments:
Post a Comment