Arusha
Wanunuzi wa madini kutoka maeneo mbalimbali nchini wameendelea kujitokeza katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) jijini Arusha, wakikagua na kuhakiki ubora wa madini yatakayouzwa katika Mnada wa Tatu wa Madini ya Vito unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2025.
Ukaguzi huo ni hatua muhimu inayolenga kuhakikisha uwazi, ushindani na ongezeko la thamani ya madini nchini, kwa kuwa madini yote yatakayopatikana kwenye mnada huo wa kidigitali lazima yakidhi viwango na thamani halisi ya soko.
Mnada huo umeendelea kuvutia wanunuzi wengi wa ndani, jambo linalopanua fursa za kibiashara na kuimarisha mchango wa sekta ya madini katika ukuaji wa uchumi wa taifa.
Aidha, unafungua milango kwa wachimbaji na wauzaji kuongeza wigo wa soko kupitia mfumo wa kisasa na salama wa uuzaji.










No comments:
Post a Comment