ZUNGU ACHAGULIWA KUWA SPIKA MPYA WA BUNGE LA TANZANIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 11, 2025

ZUNGU ACHAGULIWA KUWA SPIKA MPYA WA BUNGE LA TANZANIA



Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA


Aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu, amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 378 kati ya kura 383 zilizopigwa, huku kura tatu zikiharibika.

Mheshimiwa Zungu amewashinda wagombea wengine wakiwemo Ndg. Veronica Charles Tyeah kutoka Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Ndg. Anitha Alfan Mgaya kutoka Chama cha National League for Democracy (NLD), Ndg. Chrisant Nyakitita kutoka Chama cha Democratic Party (DP), Ndg. Ndonge Said Ndonge kutoka Chama cha Alliance for Africa Farmers Party (AAFP), na Ndg. Amin Alfred Yango kutoka Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).

No comments:

Post a Comment